Njia Ya Uzima
Scheduled on
Saturday | 20:00 | 21:00 | |
---|---|---|---|
Saturday | 20:00 | 20:00 |
Njia Ya Uzima (Path to Life)
Ni kipindi cha neno la Mungu chenye lengo la kuwafikia watu wote wanaosikia na kuelewa lugha ya kiswahili popote duniani. Kipindi hiki kimesheheni Nyimbo za injili ,Neno la Mungu, shuhuda, madokezo ya muhimu kuhusu ufalme wa Mungu, maombi na maombezi na mambo mengi ya kukujenga katika kuishi maisha sawasawa na mapenzi ya Mungu. Kipindi kimeandaliwa na huduma ya eChurch Global kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Makao makuu ya huduma ni Stjørdal Norway.
Huduma ya eChurch Global ni huduma ya kupeleka injili (Habari Njema) mpaka kiganjani kwako kwa njia ya mtandao. Msingi wetu umejengwa kupitia (Mathayo 28 : 19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu) . Baadhi ya majukwaa ya mitandao tunayotumia ni YouTube, Facebook, Instagram na Twitter jina ni ¨eChurch Global¨
Huduma pia inahudumia watu mbalimbali wenye uhitaji kama yatima, wajane, wagane, watoto wa mitaani nchini Tanzania n.k. Pia huduma inasaidia kwa hali na mali watumishi wengine katika kupeleka injili ya Yesu vijijini (Tanzania)
Unaweza kushiriki nasi baraka hizi kwa sadaka yako na tunakukaribisha kujiunga nasi (Tuna kikundi cha whatsapp kinaitwa Friends and Partners of eChurch Global mlango uko wazi kwajili yako pia)
Karibu wasiliana nasi kupitia: echurch.global@gmail.com
Lead Minister, Richard Rwechungura, PhD
Whatsapp +4791706974 au +255656566534 au +255757564612 au +4792055506 au +255674698865
MEDIA Links
YouTube: https://www.youtube.com/channel/UC14uzUMtLnro3BOdS11blKQ/videos
Facebook: https://www.facebook.com/E-Church-Global-110100870547460
Instagram: https://www.instagram.com/echurch_global/
Twitter: https://twitter.com/EchurchGlobal
Read more
Podcast of previous episodes
Sorry, there is nothing for the moment.
Related news
Sorry, there is nothing for the moment.